Simulizi ya Dimbwi la damu.
nchi hiyo, ilikuwa ni tenda ya mamilioni ya dola za kimarekani na ilikuwa ni kazi kubwa kuliko kazi zote alizowahi kufanya tangu akabidhiwe kampuni.Wafanyabiashara wengi nchini Canada waliitaka kazi hiyo na kampuni ya Canada Oils& Gas nayo ilikuwa miongoni mwa kampuni zilizoiomba. “Mama ni lazima tufanye lolote linalowezekana kuhakikisha tunapata tenda hii?” “Fanya lolote mwanangu, kila kitu ni ruksa!” “Ni lazima tutumie pesa mama! Sababu wanasema tumia pesa ili upate pesa!” “Sawa tu mwanangu!” Hilo ndilo alilofanya Manjit, alitumia pesa nyingi kuwahonga watu wote waliokuwa na mamlaka ya kuitoa tenda mpaka akaibuka mshindi! Ilikuwa ni furaha kubwa mno kwa Manjit, mama yake, Victoria na hata wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo! Walijua kupatikana kwa kazi hiyo kungeongeza maslahi yao. “Mama tumetajirika!” “Hakika mwanangu! Nimeamini una akili” “Itabidi nisafiri hadi Iran kwenda kuongea biashara na matajiri wa huko ikiwezekana tuwe tunapata mafuta ya mkopo kutoka kwao na kuwalipa b