Mwandaaji wa makala hii EmmanuelKasomi Kama kuna mwanamuziki ambaye hawezi kusahaulika katika kumbukumbu za wapenda muziki, ni Dk. Remmy Ongalla. Sasa ni miaka kadhaa tangu aiage dunia, baada ya kufariki dunia usiku wa kuamkia Jumatatu Desemba 13, 2010 nyumbani kwake Sinza, jijini Dar es Salaam. Ilikuwa ni siku ya majonzi kwa wapenzi wa muziki wa dansi hapa Tanzania, Afrika ya Mashariki na Ulimwenguni kwa ujumla baada ya kusikika kwa kifo chake. Kifo cha Dk. Remmy kiliwaacha wapenzi wake na wananchi kwa ujumla katika dimbwi la majonzi yasiyosahaulika kufuatia tungo za nyimbo zake zenye maudhui maridhawa, ambazo hadi leo zinarindima katika vituo vingi vya redio hapa nchini hata nje ya mipaka yetu. Yapo mambo kadhaa aliyoyafanya ambayo yanasababisha watu wengi kutokumsahau nguli huyu. Dk. Remmy alikuwa wa kwanza kupata ujasiri wa kukemea ngono zembe, akatunga wimbo ‘Mambo kwa soksi’ Lakini jamii ikambeza kwamba wimbo huo haukuwa na maadili mema. Baadaye viongozi wa serikali, vyama na din
Leo nakurejeshea kesi ya Bi. Sarah Simbaulanga lakini leo utaifahamu kwa uzuri yaani kutoka Mwanzo Mwisho. Na Emmanuel Kasomi IPO HIVI Saa 7 kamili mchana, siku ya jumapili ya tarehe 1.11.1987, Watanzania, kila pembe ya nchi, walipigwa butwaa na kushikwa na bumbuwazi kubwa baada ya Radio Tanzania Dar Es Salaam kutangaza, katika taarifa ya habari, kwamba mwanamke aitwae SARAH MARTIN SIMBAULANGA (35) mfanyakazi wa NBC alikuwa amekwapua mamilioni ya fedha na alitoroka nchini akiwa na watoto wake watatu na laaziz wake, Mfanyabiashara TOROHA MOHAMED TOROHA(40). Tukio hilo la kipekee na la aina yake liliwaacha midomo wazi wananchi hasa kwavile enzi hizo halikuwa jambo la kawaida kwa mwanamke kuwa "mpigaji" wa kiwango cha kutisha cha fedha nyingi kiasi kile!. Tukio hilo liliongelewa mno sehemu mbalimbali hasa maofisini, majumbani, mashuleni, masokoni, mahotelini, vilabuni nk huku wengi wakimlaani vikali mwanamke huyo na kusikitika nchi kuibiwa fedha nyingi kiasi hicho. Kwa wen
Tarehe 2 January mwaka 1845, mwanadada Mary Moffat alifunga ndoa na kijana David katika harusi iliyofanyika huko nchini Afrika Kusini. Mary ni mtoto wa kwanza kati ya watoto kumi wa mzee Robert Moffat, raia wa Scotland aliyekuja Afrika kusini kufanya kazi ya umishionari na kuwa mtu wa kwanza kutafsiri biblia kwenda katika lugha ya setswana inayozunguzwa na watu wa Botswana na baadhi ya waafrika Kusini. Mary Moffat kama anavyoonekana upande wa kulia pichani, alizaliwa mwaka 1821 huko nchini Afrika Kusini akichukua jina la mama yake ambaye naye anaitwa Mary Smith. Mwaka 1839 aliondoka pamoja na wazazi wake kurudi Uingereza na kukaa huko hadi mwaka 1843 waliporudi tena nchini Afrika Kusini katika eneo linaloitwa Kuruman. Hapa ndio kituo cha kwanza cha wamishenari wa shirika la 'London Missionary Society LMS' na moja kati ya vitu vilivyowafanya LMS waje hapa ni ile bwawa la chemchem ya maji safi iliyopewa jina la 'Jicho la Kuruman' aliyekuwa chifu wa eneo lile 'kuruma
Comments
Post a Comment