Stori ya John na Jeany (By Dizasta vina)
John alimpenda sana Jenny, licha ya umaskini aliokuwa nao alijitahidi sana kumpa Jenny kila alichokitaka. John alijua kabisa kuwa Jenny hakumpenda, lakini bado alijitahidi kufanya kila alichoweza ila kum impress Jenny. Malengo yake ilikua ni kuja kumpa mwanamke huyo magari na majumba, na badala yake akaishia kumudu kumnunulia chai, chipsi mayai na vocha. Pamoja na jitihada zake zote, John kila alipomwambia Jenny kuwa anampenda hakuwahi kujibiwa! Jambo hilo lilimuumiza sana John, lakini bado akaendelea kusubiri kwani “atafutae hachoki”. Pamoja na yote John alijua sababu ya Jenny kutokumpenda sawa na yeye anavyompenda..Jenny alizaliwa kwenye familia maskini sana. Umaskini huo umemuumiza sana na nd'o chanzo cha kifo cha mama yake kufariki kwa kukosa matibabu. Na hii ndo sababu Jenny akaweka nadhiri ya kuwa hatokubali kuishi katika umaskini, na nadhiri hiyo ndiyo chanzo cha mateso ya John. Jenny aliuchukia umaskini na asingeweza kusubiri hustle za John zilipe. Alimuomba Mungu John ‘ao