Jinsi ya kutengeneza You Tube channel
Jinsi ya kufungua akaunti ya Youtube 1. Anza kwa Jisajili kwenye akaunti ya Google (Kama hauna) Ili kuweza kuangalia maudhui ya video kwenye YouTube, kutenegeneza akaunti ya YouTube, kushare, kutoa maoni (comments) unapaswa kuwa na akaunti ya Google. Jinsi ya kusajili akaunti ya Google (Googgle account) kama hauna akaunti Nenda kwenye youtube.com na bofya “ingia”(Sign in) kwenye kona ya juu ya mkono wa kulia. Kutoka huko, utapelekwa kwenye ukurasa wa kuingia katika Google. Bonyeza “chaguo zaidi” (More Options). Kisha tengeneza akaunti yako ya Google Ukitoka hapa utapaswa kufuata hatua chache ili kuunda akaunti ya Google. Mara baada ya kuzikamilisha, endelea hatua zifuatazo. Ikiwa Unayo Tayari Akaunti ya Google Nenda kwenye youtube.com na bofya “ingia” kwenye kona ya juu ya mkono wa kulia. Kutoka huko, utachukuliwa kwenye ukurasa huo huo wa Google wa kuingia. Ikiwa una akaunti nyingi za Google, hakikisha unachagua moja unayotaka ...