Historia ya Nyerere
Nifanyeje
Cheo : Raisi wa Zamani
Julius Kambarage Nyerere
Utumishi:
1962 - 1985 (Rais wa Tanzania)
Taarifa za Kina
Tarehe ya Kuzaliwa: 1922-04-13
Mahali pa Kuzaliwa: Butiama - Musoma
Ndoa: Ameoa
Utumishi:
1962 - 1985 (Rais wa Tanzania)
Taarifa za Kina
Tarehe ya Kuzaliwa: 1922-04-13
Mahali pa Kuzaliwa: Butiama - Musoma
Ndoa: Ameoa
Maelezo
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania alizaliwa tarehe 13 Aprili, mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma katika Mkoa wa Mara. Alikuwa mtoto wa Chifu Nyerere Burito na Bibi Christina Mugaya Wanyang’ombe. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata elimu ya msingi katika shule ya Mwisenge iliyoko katika Manispaa ya Musoma na baadaye akaendelea na masomo katika shule ya Tabora. Alisomea shahada ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda mwaka 1943-45 na mwaka 1952 alihitimu shahada ya uzamili katika masomo ya Historian a Uchumi Edinburgh, Uingereza. Kabla ya kuanza harakati za kisiasa Mwalimu Nyerere alifundisha katika shule za sekondari za Tabora na St. Francis ambayo sasa inaitwa Pugu Sekondari.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na viongozi wenzake wa awamu ya kwanza walielekeza juhudi zao katika kuwaunganisha Watanzania na kuweka misingi imara ya kuijenga taifa; kudumisha uhuru na amani na kuweka itikadi na sera za kukabili ujinga, umaskini na maradhi. Aidha, awamu hii iliweka misingi madhubuti ya uhusiano wa nje ikiwa ni pamoja na sera ya kutofungamana na siasa za upande wowote, msisitizo katika ukombozi wa Bara la Afrika na mapambano dhidi ya ubeberu na vibaraka wao. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Azimio la Arusha lililosisitiza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni matunda ya uongozi wa awamu ya kwanza. Mwalijmu Julius Kambarage Nyerere alifariki dunia katika hospitali ya Mtakatifu Thomas iliyoko mjini London, Uingereza tarehe 14 Oktoba, 1999. Kutokana na mchango wake mkubwa kama muasisi wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere ataendelea kukumbukwa kuwa Baba wa Taifa.
Viongozi Mashuhuri
Katiba
Mpangilio Orodha
Bunge
Taratibu na Kanuni
Gazeti la Serikali
Sheria
Mipango ya Maendeleo
Sera
Wafanyakazi
Takwimu
Ulinzi na Usalama
Nyaraka
Mahakama
Bajeti
Vijarida Mtandao
Miundo ya Utumishi
Fomu
Kanuni na sheria
Tovuti Kuu ya Serikali Imesanifiwa, imetengenezwa na inahifadhiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao. Taarifa zinasimamiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Lengo kuu la Tovuti Kuu hii ni kuwezesha upatikanaji wahuduma za umma kwa uwazi, urahisi na gharama nafuu kutoka Taasisi mbalimbali za umma kwa manufaa ya wananchi, wafanyabiashara, watumishi na wadau wengine wandani na nje ya nchi. Taarifa zilizomo ndani ya Tovuti Kuu hii ni matokeo ya juhudi za pamoja za Taasisi mbalimbali
Comments
Post a Comment