Historian ya Ginimbi
Genius Ginimbi Kadungure: Mfahamu milionea wa Zimbabwe aliyefariki katika ajali ya barabarani
Genius Kadungure maarufu Ginimbi alikuwa mtu maarufu sana nchini Zimbabwe akiwa mlimbwende na mfanyabiashara.
Pia alikuwa mwanzilishi wa kampuni ya bkuuza gesi ya Pioneer gases ambayo ina kampuni nchini Botswana , Afrika Kusini na Zimbabwe. Mnamo tarehe 8 mwezi Novemba 2020, Ginimbi aliaga dunia baada ya ajali ya gari .
Gari hilo aina ya Rolls Royce lilidaiwa kugonga gari jingine na kukosa mwelekeo na kugonga mtu kandokando ya barabara. Kufuatia hatua hiyo gari hili liliwaka moto na kuchomeka.
Kulingana na mashahidi Ginimbi alidaiwa kutolewa akiwa hai lakini akafariki muda mchache baadaye. Abiria wengine wawili waliokuwa ndani walisalia ndani yake na kuchomeka hadi mauti yao.
Maisha ya utoto wake
Genius kadungure alizaliwa tarehe 10 mwezi Oktoba 1984 katika eneo la Domboshava katika familia ya watu wanne.
Alikuwa akiitwa jina Ginimbi jina ambalo alilitumia katika akaunti yake ya facebook.
Biashara
Kadungure alidaiwa kuanza biashara ndogo ndogo akiwa na umri wa miaka 17 huku akiwa wakala wa gesi .
Alianzisha kampuni ya gesi ya Pioneer ambayo ni miongoni mwa makampuni ya Kundi la biashara za Piko.
Kampuni hiyo inauza gesi , kwa wafanyibiashara , kwa umma na madukani.
Maisha yake ya kibinafsi
Mwaka 2014 alidaiwa kufunga ndoa na mfanyabiashara mmoja lakini kufikia mwaka 2018 alifichua kwamba yeye na mfanyabiashara huyo wamewachana. Hatahivyo waliendelea kufanya biashara pamoja.
Sherehe za kukata na shoka
Kadungure alikuwa maarufu kama kijana aliyependa kula 'bata' na kufanya shrehe za kukata na shoka .
Mwaka 2010 , alifanya sherehe iliogharimu US$17,000 .
Sherehe hiyo ilivutia marafiki zake kutoka mji mkuu wa Harare huku wageni wakipewa mivinyo ya gharama ya juu kwa siku tatu mfululizo.
Miaka miwili baadaye 2012 alifanya sherehe nyengine ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa iliofanyika mjini Botswana .
Sherehe hiyo ilidaiwa kugharimu $32,000 wakati huo. Mwaka 2013, Kadungure alidaiwa kufanya sherehe nyengine ya siku tatu nyumbani kwao huko Domboshava ili kusherehekea jumba lake jipya katika eneo hilo.
Mipango ya mazishi
Kulingana na mtandao wa Zimbabwe Cronicles , mwili wa Genius Kadungure utawasili nyumbani kwake siku ya Jumamosi alfajiri .
Kulingana na mtandao huo ndugu yake Clement Kadungure ambaye alinukuliwa akisema kwamba, kutakuwa na ibada ya wafu ambapo watu wa karibu wa marehemu watazungumza.
Mwili wake baadaye utazikwa nyumbani kwake na sio ndani ya nyumba yake kama inavyoarifiwa na baadhi ya watu.
Kulingana na bwana Clement atazikwa kulingana na tamaduni za jamii yake.
Vilvile alipinga madai kwamba kutakuwa na sherehe ya kuvaa mavazi meupe akisisitiza kwamba yatakuwa mazishi na sio sherehe, hivyobasi wanaotaka kuvalia mavazi hayo watafanya hivyo kwa hiari yao.








Comments
Post a Comment