Stori ya John na Jeany (By Dizasta vina)

 John alimpenda sana Jenny, licha ya umaskini aliokuwa nao alijitahidi sana kumpa Jenny kila alichokitaka. John alijua kabisa kuwa Jenny hakumpenda, lakini bado alijitahidi kufanya kila alichoweza ila kum impress Jenny. Malengo yake ilikua ni kuja kumpa mwanamke huyo magari na majumba, na badala yake akaishia kumudu kumnunulia chai, chipsi mayai na vocha.




Pamoja na jitihada zake zote, John kila alipomwambia Jenny kuwa anampenda hakuwahi kujibiwa! Jambo hilo lilimuumiza sana John, lakini bado akaendelea kusubiri kwani “atafutae hachoki”.




Pamoja na yote John alijua sababu ya Jenny kutokumpenda sawa na yeye anavyompenda..Jenny alizaliwa kwenye familia maskini sana. Umaskini huo umemuumiza sana na nd'o chanzo cha kifo cha mama yake kufariki kwa kukosa matibabu. Na hii ndo sababu Jenny akaweka nadhiri ya kuwa hatokubali kuishi katika umaskini, na nadhiri hiyo ndiyo chanzo cha mateso ya John.




Jenny aliuchukia umaskini na asingeweza kusubiri hustle za John zilipe. Alimuomba Mungu John ‘aokote' utajiri na alivyoona hilo halikaribii kutokea akaamua kuchukua hamsini zake.




Jenny akapata bwana wa kizungu, bwana ambaye angeweza kumfanya aishi maisha aliyoyataka. Japo jamb hilo lilimuumiza John hadi kufikia hatua akawa ‘mwendawazimu' na kupoteza kabisa muelekeo wa maisha yake lakin hakuona kama ni sahihi kumlazimisha Jenny abaki kwani yeye aliamini kuwa ukilipenda ua sio lazima ulikate,liache likue. Jenny akaenda zake Miami kufuata ndoto zake, kuufuata utajiri aliohusudu.. Na john akabaki na upendo wake.




Kitendo cha Jenny kuondoka kilimuachia John maumivu makali ambayo yalichelewa sana kupona kiasi kwamba akaweka nadhiri kuwa kamwe asingejihusicha tena na mapenzi. Lakini kama tujuavyo, muda ni daktari mzuri zaidi! Baada ya miaka kadhaa kupita John akasahau (au akafikiri amesahau) kuhusu Jenny. Akapata msichana mwingine ambaye japo yeye (John) hakumpenda ila yeye alimpenda na alijitoa sana na hivyo ikambid John ajifunze kumjali.




Mapenzi ya John na huyo mwanamwali yakafikia hatua ambayo wakakubaliana kufunga ndoa. Michango ikaanza na maandalizi yakapamba moto, lakini haikua mpaka pale ambapo John alipopokea ujumbe kutoka kwa Jenny kupitia mtandao wa kijamii. Ujumbe huo ukamkumbusha kuwa sio kweli kuwa amemsahau Jenny kama ambavyo yeye alifikiri:




“Habari naamini u bukheri wa afya




Unaendeleaje maisha na huyo mpenzi wa sasa?




nashukuru nahema, ughaibuni si kwema


Nakiona cha mtema mpaka naona ni heri nikafa…




Maisha niliyowaza yote ni uongo


Nauzishwa madawa nalazimishwa ngono


Nafungiwa ndani kama mtumwa ufungwani




Roho yangu rehani kiasi sasa naitamani Bongo




Ukubwa umekuja kunisafisha jicho


Ndoto imeisha na taswira imenionyesha sivyo,




Naomba unifate uniondoshe kwenye hiki kifo




Na hii namba ya msamaria atakueleza nilipo”






Ni kweli kuwa John alimpenda sana Jenny na kamwe hakuwahi kumsahau! Kitu ambacho hakujua ni kuwa Jenny hakumpenda kama yeye alivyompenda. Akaamua kubeba pesa za michango ya harusi ambazo tayari ametolewa kwa ajili ya harusi yake na ‘mwanamwali'. John akaianza safari yake kuelekea ughaibuni kumfuata “njiwa” wake…


Imeletwa kwenu na Emmanuel kasomi

Comments

Popular posts from this blog

Historia Ya Remmy Ongala

Mfahamu Sarah Martin Simbaulanga

Historia ya Dr. Livingstone