Posts

Stori ya John na Jeany (By Dizasta vina)

 John alimpenda sana Jenny, licha ya umaskini aliokuwa nao alijitahidi sana kumpa Jenny kila alichokitaka. John alijua kabisa kuwa Jenny hakumpenda, lakini bado alijitahidi kufanya kila alichoweza ila kum impress Jenny. Malengo yake ilikua ni kuja kumpa mwanamke huyo magari na majumba, na badala yake akaishia kumudu kumnunulia chai, chipsi mayai na vocha. Pamoja na jitihada zake zote, John kila alipomwambia Jenny kuwa anampenda hakuwahi kujibiwa! Jambo hilo lilimuumiza sana John, lakini bado akaendelea kusubiri kwani “atafutae hachoki”. Pamoja na yote John alijua sababu ya Jenny kutokumpenda sawa na yeye anavyompenda..Jenny alizaliwa kwenye familia maskini sana. Umaskini huo umemuumiza sana na nd'o chanzo cha kifo cha mama yake kufariki kwa kukosa matibabu. Na hii ndo sababu Jenny akaweka nadhiri ya kuwa hatokubali kuishi katika umaskini, na nadhiri hiyo ndiyo chanzo cha mateso ya John. Jenny aliuchukia umaskini na asingeweza kusubiri hustle za John zilipe. Alimuomba Mungu John ‘ao...

MO Dewj Billionea wa 13 Afrika

Image
Katika orodha hiyo ya jarida mashuhuri la Forbes linalofuatilia utajiri wa watu kwa mwaka huu limemtaja Mo mwenye miaka 45 kama bilionea namba 13 akitoka nafasi ya 17 mwaka jana huku mfanyabiashara wa saruji, sukari na unga (Aliko Dangote wa Nigeria) akiendelea kuongoza orodha hiyo. Inaelezwa kuwa utajiri wa Mo wa sasa ni Dola za Marekani bilioni 1.6 (Sh3.7 trilioni) na anayeshikilia namba moja utajiri wake ni Dola 12.1 bilioni (Sh28.9 trilioni). Katika orodha ya jarida hilo ya Januari mwaka jana, Mo anayefanya biashara mchanganyiko alikuwa nafasi ya 17 akiwa na utajiri huohuo wakati mwaka juzi alishika nafasi ya 14 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.9. Mwaka jana baada ya utajiri wake kupungua kwa Dola milioni 300 (Sh695.7 bilioni) na kushuka nafasi tatu katika orodha ya matajiri Afrika alilieleza gazeti hili kuwa mwaka ulioisha ungekuwa wa neema. “Imepungua Dola milioni 300 (Sh692.67 bilioni ya wakati huo), lakini nina watu 32,000 na mwaka huu natarajia kuwekeza Sh500 bilioni hapahap...

Historia ya Tundu A. Lissu

Image
  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu alinusurika kushambuliwa na mbunge wa zamani wa Bunda, Steven Wasira katika moja ya vikao vya Bunge mjini Dodoma. Lissu alisema hayo wakati akisimulia sehemu ya maisha yake binafsi na mambo aliyowahi kukutana nayo maishani katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika Jumatano. Katika simulizi hiyo, Lissu, ambaye kwa sasa ni rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), alizungumzia pia kesi zinazomkabili, maisha ya mahabusu, familia, kazi zake, burudani anazopenda na mahusiano yake na watu wa aina tofauti. Akizungumzia mkasa uliosababisha anusurike kupata kipigo hicho, Lissu alisema Wasira alikuwa amechukizwa na maneno yake makali bungeni. “Nilikuwa nimemuudhi kwa kumtolea maneno makali wakati nikichangia,” alisema Lissu akijaribu kukumbuka alichosema. Pamoja na kutokumbuka alichokisema, wakati huo Lissu alimponda Wasira kuwa alijiunga upinzani kwa kuwa alidhani kuna fedha na alipogundua hakuna ndipo akakimbia kurudi CCM. “Alichu...

Simulizi ya Dimbwi la damu.

  nchi hiyo, ilikuwa ni tenda ya mamilioni ya dola za kimarekani na ilikuwa ni kazi kubwa kuliko kazi zote alizowahi kufanya tangu akabidhiwe kampuni.Wafanyabiashara wengi nchini Canada waliitaka kazi hiyo na kampuni ya Canada Oils& Gas nayo ilikuwa miongoni mwa kampuni zilizoiomba. “Mama ni lazima tufanye lolote linalowezekana kuhakikisha tunapata tenda hii?” “Fanya lolote mwanangu, kila kitu ni ruksa!” “Ni lazima tutumie pesa mama! Sababu wanasema tumia pesa ili upate pesa!” “Sawa tu mwanangu!” Hilo ndilo alilofanya Manjit, alitumia pesa nyingi kuwahonga watu wote waliokuwa na mamlaka ya kuitoa tenda mpaka akaibuka mshindi! Ilikuwa ni furaha kubwa mno kwa Manjit, mama yake, Victoria na hata wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo! Walijua kupatikana kwa kazi hiyo kungeongeza maslahi yao. “Mama tumetajirika!” “Hakika mwanangu! Nimeamini una akili” “Itabidi nisafiri hadi Iran kwenda kuongea biashara na matajiri wa huko ikiwezekana tuwe tunapata mafuta ya mkopo kutoka kwao na kuwali...

Historia ya Diamond Platinumz

  Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond Platinumz (au Diomond) alianza rasmi safari yake ya muziki mwaka 2006, ingawaje hadi kufikia hapo alipo ilikuwa na changamoto nyingi.  Alilelewa na Mama na Bibi yake ambao hawakuwa na kipato kikubwa.  Alionyesha mapenzi makubwa kwenye muziki tangu akiwa na umri mdogo, kipaji chake kikiendekea kukua kwa kuiga wasanii wa ndani na nje akiimba nyimbo zao kwenye matukio mbalimbali. Baada ya kumaliza Kidato cha Nne mwaka 2006, Diamond alijikita kwenye muziki.  Diamond alipokuwa akijitahidi kujiongezea kipato kwa kuingia studio mwaka 2007, alilazimika kujiingiza kwenye ujasiriamali, kama machinga, kuajiriwa kwenye vituo vya petroli, kuwa mpiga picha wa kujitegemea na kazi nyingine yoyote ambayo aliona itamwongezea kipato.  Alifikia hatua ya kuuza vidani vya dhahabu vya mama yake kwa siri ili kuweza kulipia gharama za studio.  Hatimaye alirekodi wimbo wake wa kwanza ambao haukubamba kwenye chati sana lakini ulimfungulia mlan...

BARRIERS TO EFFECTIVE COMMUNICATION

 Barriers to Effective Communication 1. Physical Barriers Physical barriers in the workplace include: Marked out territories, empires and fiefdoms into which strangers are not allowed Closed office doors, barrier screens, and separate areas for people of different status Large working areas or working in one unit that is physically separate from others Research shows that one of the most important factors in building cohesive teams is proximity. As long as people still have a personal space that they can call their own, being close to others aids communication because it helps people get to know one another. Communicate Better and more Effectively in Just Two Days! 2. Perceptual Barriers It can be hard to work out how to improve your communication skills. The problem with communicating with others is that we all see the world differently. If we didn't, we would have no need to communicate: something like extrasensory perception would take its place. The following anecdote is a remi...

IJUE DINI YA URASTA(RASTAFARIAN)

Image
 Emmanuelkasomi nakujuza. Dini ya urasta ilianzishwa miaka ya 1920 na 1930 huko maeneo ya visiwa vya Caribbean. Mwanzilishi wa imani hii ni Marcus Garvey aliezaliwa mwaka 1887 na kufariki dunia mwaka 1940. Marasta huamini kwamba huyu jamaa ni Yohanna mbatizaji wa pili kwasababu alitoa unabii wa kutokea mfalme Afrika ambae ndie atakuwa mkombozi wa waafrika wote dhidi ya udhalimu wa mtu mweupe (Babylon). Marcus Garvey alihubiri kwamba waafrika ndio Waisrael wa Kweli waliopelekwa utumwani kama adhabu ya dhambi zao. Mnamo mwaka 1927 Marcus Garvey alitoa unabii kwamba atatokea mfalme barani Afrika ambae atakuja kuikomesha hiyo adhabu ya utumwa na kuwarudisha waafrika wote Afrika (Zion/Sayuni). Alitamka 'Look to Africa, for a king shall be crowned'. Dini ya urasta ina wafuasi zaidi ya milioni moja duniani kote. Marasta huamini katika Mungu wa kikristo anaeitwa Judeo au Jah. Marasta huyatumia maandiko ya biblia agano la kale na kitabu cha ufunuo huku wakiwatukuza sana manabii Musa na ...