Posts

Mfahamu Sarah Martin Simbaulanga

Image
  Leo nakurejeshea kesi ya  Bi. Sarah Simbaulanga    lakini leo utaifahamu kwa uzuri yaani kutoka Mwanzo Mwisho. Na Emmanuel Kasomi IPO HIVI Saa 7 kamili mchana, siku ya jumapili ya tarehe 1.11.1987, Watanzania, kila pembe ya nchi, walipigwa butwaa na kushikwa na bumbuwazi kubwa baada ya Radio Tanzania Dar Es Salaam kutangaza, katika taarifa ya habari, kwamba mwanamke aitwae SARAH MARTIN SIMBAULANGA (35) mfanyakazi wa NBC alikuwa amekwapua mamilioni ya fedha na alitoroka nchini akiwa na watoto wake watatu na laaziz wake, Mfanyabiashara TOROHA MOHAMED TOROHA(40). Tukio hilo la kipekee na la aina yake liliwaacha midomo wazi wananchi hasa kwavile enzi hizo halikuwa jambo la kawaida kwa mwanamke kuwa "mpigaji" wa kiwango cha kutisha cha fedha nyingi kiasi kile!. Tukio hilo liliongelewa mno sehemu mbalimbali hasa maofisini, majumbani, mashuleni, masokoni, mahotelini, vilabuni nk huku wengi wakimlaani vikali mwanamke huyo na kusikitika nchi kuibiwa fedha nyingi kiasi hicho...

Historia ya Msanii Grand P

Image
  Grand P Msanii Mwenye Mvuto wa Aina Yake S dd bookmark Jina la kuzaliwa:  Moussa Sanguiana Kaba  Mwaka wa kuzaliwa: 1990 Umri: Miaka 31(mwaka huu 2021) Kuzaliwa: Sanguiana (Guinea) Raia: Guinea Kipaji: Mwimbaji, muigizaji, mtu wa mitandao ya kijamii na mwanasiasa Aina ya muziki: Hip hop Miaka ya kazi: Tangu 2019 suala la kiafya: Kuugua progeria, ugonjwa adimu wa maumbile unaojulikana na kuzeeka mapema Historia zaidi na  Emmanuel Kasomi Maswali ya kujiuliza kuhusu Grand P Grand P alizaliwa lini ? -Mwanamuziki hodari wa Guinea alizaliwa mnamo 1990, ambayo inamaanisha kuwa ana umri wa miaka 31 kwa sasa. Haijulikani sana miaka ya mwimbaji mwenye talanta. Pia, yeye mara chache anashiriki habari ya familia yake. Grand P alizaliwa na ugonjwa nadra wa maumbile uitwao progeria, ambao unasababisha kuzeeka mapema ulioanza wakati wa kuzaliwa. Hali hiyo hupunguza urefu wa mtu kuwa mita mbili na uzani fulani. Msanii hodari amekuwa akidhihakiwa na kudhihakiwa kwa muda mrefu kwa s...

Stori ya John na Jeany (By Dizasta vina)

 John alimpenda sana Jenny, licha ya umaskini aliokuwa nao alijitahidi sana kumpa Jenny kila alichokitaka. John alijua kabisa kuwa Jenny hakumpenda, lakini bado alijitahidi kufanya kila alichoweza ila kum impress Jenny. Malengo yake ilikua ni kuja kumpa mwanamke huyo magari na majumba, na badala yake akaishia kumudu kumnunulia chai, chipsi mayai na vocha. Pamoja na jitihada zake zote, John kila alipomwambia Jenny kuwa anampenda hakuwahi kujibiwa! Jambo hilo lilimuumiza sana John, lakini bado akaendelea kusubiri kwani “atafutae hachoki”. Pamoja na yote John alijua sababu ya Jenny kutokumpenda sawa na yeye anavyompenda..Jenny alizaliwa kwenye familia maskini sana. Umaskini huo umemuumiza sana na nd'o chanzo cha kifo cha mama yake kufariki kwa kukosa matibabu. Na hii ndo sababu Jenny akaweka nadhiri ya kuwa hatokubali kuishi katika umaskini, na nadhiri hiyo ndiyo chanzo cha mateso ya John. Jenny aliuchukia umaskini na asingeweza kusubiri hustle za John zilipe. Alimuomba Mungu John ‘ao...

MO Dewj Billionea wa 13 Afrika

Image
Katika orodha hiyo ya jarida mashuhuri la Forbes linalofuatilia utajiri wa watu kwa mwaka huu limemtaja Mo mwenye miaka 45 kama bilionea namba 13 akitoka nafasi ya 17 mwaka jana huku mfanyabiashara wa saruji, sukari na unga (Aliko Dangote wa Nigeria) akiendelea kuongoza orodha hiyo. Inaelezwa kuwa utajiri wa Mo wa sasa ni Dola za Marekani bilioni 1.6 (Sh3.7 trilioni) na anayeshikilia namba moja utajiri wake ni Dola 12.1 bilioni (Sh28.9 trilioni). Katika orodha ya jarida hilo ya Januari mwaka jana, Mo anayefanya biashara mchanganyiko alikuwa nafasi ya 17 akiwa na utajiri huohuo wakati mwaka juzi alishika nafasi ya 14 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.9. Mwaka jana baada ya utajiri wake kupungua kwa Dola milioni 300 (Sh695.7 bilioni) na kushuka nafasi tatu katika orodha ya matajiri Afrika alilieleza gazeti hili kuwa mwaka ulioisha ungekuwa wa neema. “Imepungua Dola milioni 300 (Sh692.67 bilioni ya wakati huo), lakini nina watu 32,000 na mwaka huu natarajia kuwekeza Sh500 bilioni hapahap...

Historia ya Tundu A. Lissu

Image
  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu alinusurika kushambuliwa na mbunge wa zamani wa Bunda, Steven Wasira katika moja ya vikao vya Bunge mjini Dodoma. Lissu alisema hayo wakati akisimulia sehemu ya maisha yake binafsi na mambo aliyowahi kukutana nayo maishani katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika Jumatano. Katika simulizi hiyo, Lissu, ambaye kwa sasa ni rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), alizungumzia pia kesi zinazomkabili, maisha ya mahabusu, familia, kazi zake, burudani anazopenda na mahusiano yake na watu wa aina tofauti. Akizungumzia mkasa uliosababisha anusurike kupata kipigo hicho, Lissu alisema Wasira alikuwa amechukizwa na maneno yake makali bungeni. “Nilikuwa nimemuudhi kwa kumtolea maneno makali wakati nikichangia,” alisema Lissu akijaribu kukumbuka alichosema. Pamoja na kutokumbuka alichokisema, wakati huo Lissu alimponda Wasira kuwa alijiunga upinzani kwa kuwa alidhani kuna fedha na alipogundua hakuna ndipo akakimbia kurudi CCM. “Alichu...

Simulizi ya Dimbwi la damu.

  nchi hiyo, ilikuwa ni tenda ya mamilioni ya dola za kimarekani na ilikuwa ni kazi kubwa kuliko kazi zote alizowahi kufanya tangu akabidhiwe kampuni.Wafanyabiashara wengi nchini Canada waliitaka kazi hiyo na kampuni ya Canada Oils& Gas nayo ilikuwa miongoni mwa kampuni zilizoiomba. “Mama ni lazima tufanye lolote linalowezekana kuhakikisha tunapata tenda hii?” “Fanya lolote mwanangu, kila kitu ni ruksa!” “Ni lazima tutumie pesa mama! Sababu wanasema tumia pesa ili upate pesa!” “Sawa tu mwanangu!” Hilo ndilo alilofanya Manjit, alitumia pesa nyingi kuwahonga watu wote waliokuwa na mamlaka ya kuitoa tenda mpaka akaibuka mshindi! Ilikuwa ni furaha kubwa mno kwa Manjit, mama yake, Victoria na hata wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo! Walijua kupatikana kwa kazi hiyo kungeongeza maslahi yao. “Mama tumetajirika!” “Hakika mwanangu! Nimeamini una akili” “Itabidi nisafiri hadi Iran kwenda kuongea biashara na matajiri wa huko ikiwezekana tuwe tunapata mafuta ya mkopo kutoka kwao na kuwali...